Maelezo la Darasa la Kiingereza ya Spring 2025
Taarifa za Msingi
Tuna madarasa ya kimsingi ya Kiingereza kwa wanafunzi ambao wanajifunza kuzungumza, kusoma na kuandika kwa Kiingereza kwa mara ya kwanza.
Tuna madarasa ya Kiingereza kwa wanafunzi ambao wamesoma Kiingereza hapo awali, lakini wanataka kuboresha Kiingereza chao.
Tuna huduma ya watoto wenye umri wa miaka 0 hadi 5.
Tuna madarasa siku 3 kwa wiki, masaa 2 kwa siku.
Gharama: Tafadhali lipa $35. Hii hutusaidia kununua vitabu na nyenzo za darasa. Ukihitaji, unaweza kulipa kwa kiasi kidogo wakati wa muhula.
Tuna madarasa katika maeneo haya na nyakati.
ALEXANDRIA
First Baptist Church of Alexandria
2932 King St, Alexandria, VA 22302
Siku: Jumanne, Jumatano, Alhamisi (siku ya pili, siku ya tatu, siku ya inne)
Wakati: Asubuhi 9:30 – 11:30
Madarasa yanaanza: Februari 4
Mwisho wa madarasa: Juni 5
Maagizo ya Usajili ya Alexandria
(1) Jaza fomu ya usajili wa wanafunzi.
Fomu ya Usajili ya Watu Wazima ya Alexandria
(2) Tutakutumia ujumbe kupanga miadi ya kukutana kwa ana.
Katika miadi, tutakuruhusu usome na kuzungumza kwa Kiingereza ili tujue ikiwa tuna darasa nzuri kwako. Pia tutakupa habari zaidi kuhusu programu yetu ya Kiingereza.
Ikiwa unazungumza Kiingereza kidogo tu, mtihani utakuwa mfupi, kama dakika 30. Ikiwa unazungumza Kiingereza kingi, mtihani litakuwa ndefu, kama saa 1.
Tunasikitika. Ulezi wetu wa watoto umejaa. Hatuwezi kuchukua watoto wapya kwa sasa.
Je, unahitaji msaada?
Tafadhali tuma ujumbe kwa 571-766-8078 na jina lako. Tutakusaidia kujiandikisha.
FAIRFAX
Redeeming Grace Church
5200 Ox Rd, Fairfax, VA 22030
Siku: Jumatatu, Jumatano, Ijumaa (siku ya kwanza, siku ya pili, Na siku ya Tano)
Muda: Saa Tatu unusu asubuhi – Saa Tano unusu asubuhi
Madarasa yanaanza: Februari 3
Kozi zinamalizika: Juni 4
Maagizo ya Usajili ya Fairfax
(1) Jaza fomu ya usajili wa wanafunzi.
Fomu ya Usajili ya Watu Wazima ya Fairfax
(2) Tafadhali njoo kwenye eneo la Fairfax wakati wa mojawapo ya nyakati hizi ili kufanya jaribio la uwekaji na ukamilishe usajili wako.
Januari 13, 12-1 jioni
Januari 15, 12-1 jioni
Januari 22, 12-1 jioni
Januari 27, 12-1 jioni